Job 16:10-13
10 aWatu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki;hunipiga shavuni mwangu kwa dharau,
na kuungana pamoja dhidi yangu.
11 bMungu amenigeuzia kwa watu wabaya,
na kunitupa katika makucha ya waovu.
12 cMambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja;
amenikamata shingo na kuniponda.
Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
13 dwapiga upinde wake wananizunguka.
Bila huruma, huchoma figo zangu,
na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
Copyright information for
SwhNEN