Job 1:6-9
Jaribu La Kwanza La Ayubu
6 aSiku moja wana wa Mungu ▼▼Wana wa Mungu hapa ina maana malaika au viumbe vya mbinguni.
walikwenda kujionyesha mbele za Bwana. Shetani ▼▼Shetani hapa ina maana ya mshtaki wa watakatifu.
naye akaja pamoja nao. 7 dBwana akamwambia Shetani, “Umetoka wapi?”Shetani akamjibu Bwana, “Natoka kuzunguka pote duniani, nikitembea huku na huko humo.”
8 eNdipo Bwana akamwambia Shetani, “Je, umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Hakuna mtu mwingine duniani aliye kama yeye, asiye na hatia, ni mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuepukana na uovu.”
9 fShetani akamjibu Bwana, “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?
Copyright information for
SwhNEN