Jeremiah 6:7-10
7 aKama vile kisima kinavyomwaga maji yake,ndivyo anavyomwaga uovu wake.
Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake,
ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.
8 bPokea onyo, ee Yerusalemu,
la sivyo nitageukia mbali nawe
na kuifanya nchi yako kuwa ukiwa,
asiweze mtu kuishi ndani yake.”
9Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenye Nguvu Zote:
“Wao na wayakusanye mabaki ya Israeli
kwa uangalifu kama kwenye mzabibu;
pitisha mkono wako kwenye matawi tena,
kama yeye avunaye zabibu.”
10 cNiseme na nani na kumpa onyo?
Ni nani atakayenisikiliza mimi?
Masikio yao yameziba, ▼
▼Masikio yameziba kwa Kiebrania ina maana kwamba masikio yao hayajatahiriwa.
kwa hiyo hawawezi kusikia.
Neno la Bwana ni chukizo kwao,
hawalifurahii.
Copyright information for
SwhNEN