‏ Jeremiah 6:16-17

16 aHivi ndivyo asemavyo Bwana:

“Simama kwenye njia panda utazame,
ulizia mapito ya zamani,
ulizia wapi ilipo njia nzuri, uifuate hiyo,
nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
Lakini ninyi mlisema, ‘Hatutaipita hiyo.’
17 bNiliweka walinzi juu yenu na kusema,
‘Sikieni sauti ya tarumbeta!’
Lakini mkasema, ‘Hatutasikiliza.’
Copyright information for SwhNEN