‏ Jeremiah 51:44-58

44 aNitamwadhibu Beli katika Babeli,
na kumfanya atapike kile alichokimeza.
Mataifa hayatamiminika tena kwake.
Nao ukuta wa Babeli utaanguka.

45 b“Tokeni ndani yake, enyi watu wangu!
Okoeni maisha yenu!
Ikimbieni hasira kali ya Bwana.
46 cMsikate tamaa wala msiogope tetesi
zitakaposikika katika nchi;
tetesi moja inasikika mwaka huu,
nyingine mwaka unaofuata;
tetesi juu ya jeuri katika nchi,
na ya mtawala dhidi ya mtawala.
47 dKwa kuwa hakika wakati utawadia
nitakapoziadhibu sanamu za Babeli;
nchi yake yote itatiwa aibu,
na watu wake wote waliouawa
wataangukia ndani yake.
48 eNdipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake
vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli,
kwa kuwa kutoka kaskazini
waharabu watamshambulia,”
asema Bwana.

49 f“Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli,
kama vile waliouawa duniani kote
walivyoanguka kwa sababu ya Babeli.
50Wewe uliyepona upanga,
ondoka wala usikawie!
Mkumbuke Bwana ukiwa katika nchi ya mbali,
na utafakari juu ya Yerusalemu.”

51 g“Tumetahayari, kwa maana tumetukanwa
na aibu imefunika nyuso zetu,
kwa sababu wageni wameingia
mahali patakatifu pa nyumba ya Bwana.”

52 h“Lakini siku zinakuja,” asema Bwana,
“nitakapoadhibu sanamu zake,
na katika nchi yake yote
waliojeruhiwa watalia kwa maumivu makali.
53 iHata kama Babeli ikifika angani
na kuziimarisha ngome zake ndefu,
nitatuma waharabu dhidi yake,”
asema Bwana.

54“Sauti ya kilio inasikika kutoka Babeli,
sauti ya uharibifu mkuu
kutoka nchi ya Wakaldayo.
55 j Bwana ataiangamiza Babeli,
atanyamazisha makelele ya kishindo chake.
Mawimbi ya adui yatanguruma kama maji makuu,
ngurumo ya sauti zao itavuma.
56 kMharabu atakuja dhidi ya Babeli,
mashujaa wake watakamatwa,
nazo pinde zao zitavunjwa.
Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa kisasi,
yeye atalipiza kikamilifu.
57 lNitawafanya maafisa wake na wenye busara walewe,
watawala wao, maafisa, pamoja na wapiganaji wao;
watalala milele na hawataamka,”
asema Mfalme, ambaye jina lake ni Bwana Mwenye Nguvu Zote.
58 mHili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:

“Ukuta mnene wa Babeli utasawazishwa,
na malango yaliyoinuka yatateketezwa kwa moto;
mataifa yanajichosha bure,
taabu ya mataifa ni nishati tu ya miali ya moto.”
Copyright information for SwhNEN