Jeremiah 47:1-4
Ujumbe Kuhusu Wafilisti
1 aHili ndilo neno la Bwana lililomjia nabii Yeremia kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajaishambulia Gaza:2 bHili ndilo asemalo Bwana:
“Tazama jinsi maji yanavyoinuka huko kaskazini,
yatakuwa mafuriko yenye nguvu sana.
Yataifurikia nchi na vitu vyote vilivyomo ndani yake,
miji na wale waishio ndani yake.
Watu watapiga kelele;
wote waishio katika nchi wataomboleza
3 ckwa sauti ya kwato za farasi waendao mbio,
kwa sauti ya magari ya adui
na mngurumo wa magurudumu yake.
Baba hawatageuka kuwasaidia watoto wao,
mikono yao italegea.
4 dKwa maana siku imewadia
kuwaangamiza Wafilisti wote
na kuwakatilia mbali walionusurika wote
ambao wangeweza kusaidia Tiro na Sidoni.
Bwana anakaribia kuwaangamiza Wafilisti,
mabaki toka pwani za Kaftori. ▼
▼Kaftori ndio Krete.
Copyright information for
SwhNEN