Jeremiah 4:25-28
25 aNilitazama, wala watu hawakuwepo;kila ndege wa angani alikuwa ameruka zake.
26Nilitazama, hata nchi iliyokuwa imestawi vizuri imekuwa jangwa,
miji yake yote ilikuwa magofu
mbele za Bwana,
mbele ya hasira yake kali.
27 bHivi ndivyo Bwana asemavyo:
“Nchi yote itaharibiwa,
ingawa sitaiangamiza kabisa.
28 cKwa hiyo dunia itaomboleza
na mbingu zilizo juu zitakuwa giza,
kwa sababu nimesema nami sitarudi nyuma,
nimeamua na wala sitageuka.”
Copyright information for
SwhNEN