Jeremiah 31:35-36
35 aHili ndilo asemalo Bwana,yeye aliyeweka jua
liwake mchana,
yeye anayeamuru mwezi na nyota
kungʼaa usiku,
yeye aichafuaye bahari
ili mawimbi yake yangurume;
Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake:
36 b“Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni pangu,”
asema Bwana,
“ndipo wazao wa Israeli watakoma
kuwa taifa mbele yangu daima.”
Copyright information for
SwhNEN