‏ Jeremiah 31:31-34

31 a“Siku zinakuja,” asema Bwana,
“nitakapofanya agano jipya
na nyumba ya Israeli
na nyumba ya Yuda.
32 bHalitafanana na agano
nililofanya na baba zao
wakati nilipowashika mkono
kuwaongoza watoke Misri,
kwa sababu walivunja agano langu,
ijapokuwa nilikuwa mume kwao,”
asema Bwana.
33 c“Hili ndilo agano nitakalofanya na nyumba ya Israeli
baada ya siku zile,” asema Bwana.
“Nitaweka sheria yangu katika nia zao,
na kuiandika mioyoni mwao.
Nitakuwa Mungu wao,
nao watakuwa watu wangu.
34 dMtu hatamfundisha tena jirani yake,
wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Bwana Mungu,’
kwa sababu wote watanijua mimi,
tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,”
asema Bwana.
“Kwa sababu nitasamehe uovu wao,
wala sitazikumbuka dhambi zao tena.”
Copyright information for SwhNEN