‏ Jeremiah 30:18-19

18 a“Hili ndilo asemalo Bwana:

“ ‘Nitarudisha baraka za mahema ya Yakobo,
na kuhurumia maskani yake.
Mji utajengwa tena juu ya magofu yake,
nalo jumba la kifalme litasimama mahali pake halisi.
19 bNyimbo za kushukuru zitatoka kwao
na sauti ya furaha.
Nitaiongeza idadi yao
wala hawatapungua,
nitawapa heshima
na hawatadharauliwa.
Copyright information for SwhNEN