Jeremiah 23:21-27
21 aMimi sikuwatuma manabii hawa,lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.
Mimi sikusema nao,
lakini wametabiri.
22 bLakini kama wangesimama barazani mwangu,
wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu,
nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya
na kutoka matendo yao maovu.”
23 c“Je, mimi ni Mungu aliyeko hapa karibu tu,”
Bwana asema,
“wala si Mungu aliyeko pia mbali?
24 dJe, mtu yeyote aweza kujificha
mahali pa siri ili nisiweze kumwona?”
Bwana asema.
“Je, mimi sikuijaza mbingu na nchi?”
Bwana asema.
25 e“Nimesikia wanayoyasema manabii, hao wanaotabiri uongo kwa jina langu. Wanasema, ‘Nimeota ndoto! Nimeota ndoto!’ 26 fMambo haya yataendelea mpaka lini ndani ya mioyo ya hawa manabii wa uongo, ambao hutabiri maono ya uongo ya akili zao wenyewe? 27 gWanadhani ndoto wanazoambiana wao kwa wao zitawafanya watu wangu walisahau jina langu, kama baba zao walivyolisahau jina langu kwa kumwabudu Baali.
Copyright information for
SwhNEN