Jeremiah 23:16-21
16 aHili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo:“Msisikilize wanachowatabiria manabii,
wanawajaza matumaini ya uongo.
Wanasema maono kutoka akili zao wenyewe,
hayatoki katika kinywa cha Bwana.
17 bHuendelea kuwaambia wale wanaonidharau mimi,
‘Bwana asema: Mtakuwa na amani.’
Kwa wale wote wafuatao ugumu wa mioyo yao,
wao husema, ‘Hakuna dhara litakalowapata.’
18 cLakini ni yupi miongoni mwao aliyesimama katika baraza la Bwana
ili kuona au kusikia neno lake?
Ni nani aliyesikiliza
na kusikia neno lake?
19 dTazama, dhoruba ya Bwana
itapasuka kwa ghadhabu,
kisulisuli kitazunguka na kuanguka
vichwani vya waovu.
20 eHasira ya Bwana haitageuka mpaka amelitimiza kusudi la moyo wake.
Siku zijazo mtalifahamu kwa wazi.
21 fMimi sikuwatuma manabii hawa,
lakini bado wamekimbia wakitangaza ujumbe wao.
Mimi sikusema nao,
lakini wametabiri.
Copyright information for
SwhNEN