Jeremiah 16:19-21
19 aEe Bwana, nguvu zangu na ngome yangu,kimbilio langu wakati wa taabu,
kwako mataifa yatakujia
kutoka miisho ya dunia na kusema,
“Baba zetu hawakuwa na chochote zaidi ya miungu ya uongo,
sanamu zisizofaa kitu
ambazo hazikuwafaidia lolote.
20 bJe, watu hujitengenezea miungu yao wenyewe?
Naam, lakini hao si miungu!”
21 c“Kwa hiyo nitawafundisha:
wakati huu nitawafundisha
nguvu zangu na uwezo wangu.
Ndipo watakapojua
kuwa Jina langu ndimi Bwana.
Copyright information for
SwhNEN