‏ Jeremiah 12:4-11

4 aJe, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,
na majani katika kila shamba kunyauka?
Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,
wanyama na ndege wameangamia.
Zaidi ya hayo, watu wanasema,
Bwana hataona yatakayotupata sisi.”

Jibu La Mungu

5 b“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,
unawezaje kushindana na farasi?
Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,
utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?
6 cNdugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:
hata wao wamekusaliti;
wameinua kilio kikubwa dhidi yako.
Usiwaamini, ingawa wanazungumza
mema juu yako.

7“Nitaiacha nyumba yangu,
nitupe urithi wangu;
nitamtia yeye nimpendaye
mikononi mwa adui zake.
8 dUrithi wangu umekuwa kwangu
kama simba wa msituni.
Huningurumia mimi,
kwa hiyo ninamchukia.
9 eJe, urithi wangu haukuwa
kama ndege wa mawindo wa madoadoa
ambaye ndege wengine wawindao
humzunguka na kumshambulia?
Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;
walete ili wale.
10 fWachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu
na kulikanyaga shamba langu;
watalifanya shamba langu zuri
kuwa jangwa la ukiwa.
11 gLitafanywa kuwa jangwa,
lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;
nchi yote itafanywa jangwa
kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.
Copyright information for SwhNEN