Jeremiah 11:20-23
20 aLakini, Ee Bwana Mwenye Nguvu Zote, wewe uhukumuye kwa haki,nawe uchunguzaye moyo na akili,
wacha nione ukiwalipiza wao kisasi,
kwa maana kwako nimeweka shauri langu.
21 b“Kwa hiyo hili ndilo Bwana asemalo kuhusu watu wa Anathothi wale wanaotafuta uhai wako wakisema, ‘Usitoe unabii kwa jina la Bwana, la sivyo utakufa kwa mikono yetu’: 22 ckwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: ‘Nitawaadhibu. Vijana wao waume watakufa kwa upanga, wana wao na binti zao kwa njaa. 23 dHawatasaziwa hata mabaki kwao, kwa sababu nitaleta maafa kwa watu wa Anathothi katika mwaka wa adhabu yao.’ ”
Copyright information for
SwhNEN