‏ Jeremiah 10:3-10

3 aKwa maana desturi za mataifa hazina maana,
wanakata mti msituni,
na fundi anauchonga kwa patasi.
4 bWanaparemba kwa fedha na dhahabu,
wanakikaza kwa nyundo na misumari ili kisitikisike.
5 cSanamu zao ni kama sanamu
iliyowekwa shambani la matango kutishia ndege
nazo haziwezi kuongea;
sharti zibebwe
sababu haziwezi kutembea.
Usiziogope; haziwezi kudhuru,
wala kutenda lolote jema.”

6 dHakuna aliye kama wewe, Ee Bwana;
wewe ni mkuu,
jina lako ni lenye nguvu katika uweza.
7 eNi nani ambaye haimpasi kukuheshimu wewe,
Ee Mfalme wa mataifa?
Hii ni stahili yako.
Miongoni mwa watu wote wenye hekima
katika mataifa na katika falme zao zote,
hakuna aliye kama wewe.
8 fWote hawana akili, tena ni wapumbavu,
wanafundishwa na sanamu za miti zisizofaa lolote.
9 gHuleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi
na dhahabu kutoka Ufazi.
Kile ambacho fundi na sonara wametengeneza
huvikwa mavazi ya rangi ya samawi na urujuani:
vyote vikiwa vimetengenezwa
na mafundi stadi.
10 hLakini Bwana ni Mungu wa kweli,
yeye ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele.
Anapokasirika, dunia hutetemeka,
mataifa hayawezi kustahimili hasira yake.
Copyright information for SwhNEN