‏ Jeremiah 1:13-15

13 aNeno la Bwana likanijia tena, “Unaona nini?”

Nikajibu, “Naona chungu kinachochemka, kikiwa kimeinama kutoka kaskazini.”

14 b Bwana akaniambia, “Kutoka kaskazini maafa yatamwagwa kwa wote waishio katika nchi. 15 cNitawaita watu wote wa falme za kaskazini,” asema Bwana.

“Wafalme wao watakuja na kuweka viti vyao vya enzi
katika maingilio ya malango ya Yerusalemu,
watakuja dhidi ya kuta zake zote zinazouzunguka,
na dhidi ya miji yote ya Yuda.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.