‏ James 5:16-18

16 aKwa hiyo ungamianeni dhambi zenu ninyi kwa ninyi na kuombeana ili mpate kuponywa. Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana.

17 bEliya alikuwa mwanadamu kama sisi. Akaomba kwa bidii kwamba mvua isinyeshe, nayo haikunyesha juu ya nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita. 18 cKisha akaomba tena, nazo mbingu zikatoa mvua nayo ardhi ikatoa mazao yake.

Copyright information for SwhNEN