James 2:14-20
Imani Na Matendo
14 aNdugu zangu, yafaa nini ikiwa mtu atadai kuwa anayo imani lakini hana matendo? Je, imani kama hiyo yaweza kumwokoa? 15 bIkiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, 16 cmmoja wenu akamwambia, “Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba,” pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? 17 dVivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.18 eLakini mtu mwingine atasema, “Wewe unayo imani; mimi ninayo matendo.”
Nionyeshe imani yako pasipo matendo nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo. 19 fUnaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Vyema! Hata mashetani yanaamini hivyo na kutetemeka.
20 gEwe mpumbavu! Je, wataka kujua kwamba imani bila matendo haifai kitu?
Copyright information for
SwhNEN