Isaiah 66:2-5
2 aJe, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote,hivyo vikapata kuwepo?”
asema Bwana.
“Mtu huyu ndiye ninayemthamini:
yeye ambaye ni mnyenyekevu
na mwenye roho yenye toba,
atetemekaye asikiapo neno langu.
3 bLakini yeyote atoaye dhabihu ya fahali
ni kama yeye auaye mtu,
na yeyote atoaye sadaka ya mwana-kondoo,
ni kama yule avunjaye shingo ya mbwa.
Yeyote atoaye sadaka ya nafaka,
ni kama yule aletaye damu ya nguruwe,
na yeyote afukizaye uvumba wa kumbukumbu,
ni kama yule aabuduye sanamu.
Wamejichagulia njia zao wenyewe,
nazo nafsi zao zinafurahia machukizo yao.
4 cHivyo, mimi pia nitawachagulia mapigo makali,
nami nitaleta juu yao kile wanachokiogopa.
Kwa maana nilipoita, hakuna yeyote aliyejibu,
niliposema, hakuna yeyote aliyesikiliza.
Walifanya maovu machoni pangu
na kuchagua lile linalonichukiza.”
5 dSikieni neno la Bwana,
ninyi mtetemekao kwa neno lake:
“Ndugu zenu wanaowachukia ninyi
na kuwatenga ninyi kwa sababu ya Jina langu, wamesema,
‘Bwana na atukuzwe,
ili tupate kuona furaha yenu!’
Hata sasa wataaibika.
Copyright information for
SwhNEN