‏ Isaiah 65:13-15

13 aKwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mwenyezi:

“Watumishi wangu watakula,
lakini ninyi mtaona njaa;
watumishi wangu watakunywa
lakini ninyi mtaona kiu;
watumishi wangu watafurahi,
lakini ninyi mtaona haya.
14 bWatumishi wangu wataimba
kwa furaha ya mioyo yao,
lakini ninyi mtalia
kutokana na uchungu wa moyoni,
na kupiga yowe kwa sababu
ya uchungu wa roho zenu.
15 cMtaliacha jina lenu
kuwa laana kwa watu wangu waliochaguliwa;
Bwana Mwenyezi atawaua ninyi,
lakini watumishi wake atawapa jina jingine.
Copyright information for SwhNEN