‏ Isaiah 63:17-19

17 aEe Bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako,
na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu?
Rudi kwa ajili ya watumishi wako,
yale makabila ambayo ni urithi wako.
18 bKwa maana kwa muda mfupi watu wako walimiliki mahali pako patakatifu,
lakini sasa adui zetu wamepakanyaga mahali patakatifu pako.
19 cSisi tumekuwa kama wale ambao hujawatawala kamwe,
kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.
Copyright information for SwhNEN