Isaiah 60:4-9
4 a“Inua macho yako na utazame pande zote:
Wote wanakusanyika na kukujia,
wana wako wanakuja toka mbali,
nao binti zako wanabebwa mikononi.
5 bNdipo utatazama na kutiwa nuru,
moyo wako utasisimka na kujaa furaha,
mali zilizo baharini zitaletwa kwako,
utajiri wa mataifa utakujilia.
6 cMakundi ya ngamia yatajaa katika nchi yako,
ngamia vijana wa Midiani na Efa.
Nao wote watokao Sheba watakuja,
wakichukua dhahabu na uvumba
na kutangaza sifa za Bwana.
7 dMakundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako,
kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia,
watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu,
nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.
8 e“Ni nani hawa warukao kama mawingu,
kama hua kuelekea kwenye viota vyao?
9 fHakika visiwa vinanitazama,
merikebu za Tarshishi ▼ ndizo zinazotangulia,
zikiwaleta wana wenu kutoka mbali,
wakiwa na fedha na dhahabu zao,
kwa heshima ya Bwana, Mungu wenu,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,
kwa maana amekujalia utukufu.
Copyright information for
SwhNEN