‏ Isaiah 54:9-10


9 a“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa,
nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia.
Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi,
kamwe sitawakemea tena.
10 bIjapotikisika milima, na vilima viondolewe,
hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,
wala agano langu la amani halitaondolewa,”
asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.
Copyright information for SwhNEN