‏ Isaiah 54:10-13

10 aIjapotikisika milima, na vilima viondolewe,
hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika,
wala agano langu la amani halitaondolewa,”
asema Bwana, mwenye huruma juu yenu.

11 b“Ewe mji uliyeteswa, uliyepigwa kwa dhoruba na usiyetulizwa,
nitakujenga kwa almasi, nitaweka misingi yako kwa yakuti samawi.
12 cNitafanya minara yako ya akiki,
malango yako kwa vito vingʼaavyo,
nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
13 dWatoto wako wote watafundishwa na Bwana,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Copyright information for SwhNEN