Isaiah 54:1-4
Utukufu Wa Baadaye Wa Sayuni
1 a“Imba, ewe mwanamke tasa,wewe ambaye kamwe hukuzaa mtoto;
paza sauti kwa kuimba, piga kelele kwa furaha,
wewe ambaye kamwe hukupata utungu;
kwa sababu watoto wa mwanamke aliyeachwa ukiwa ni wengi
kuliko wa mwanamke mwenye mume,”
asema Bwana.
2 b“Panua mahali pa hema lako,
tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali,
wala usiyazuie;
ongeza urefu wa kamba zako,
imarisha vigingi vyako.
3 cKwa maana utaenea upande wa kuume
na upande wa kushoto;
wazao wako watayamiliki mataifa
na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa.
4 d“Usiogope, wewe hutaaibika.
Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa.
Wewe utasahau aibu ya ujana wako,
wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.
Copyright information for
SwhNEN