Isaiah 53:6-11
6 aSisi sote, kama kondoo, tumepotea,kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe,
naye Bwana aliweka juu yake
maovu yetu sisi sote.
7 bAlionewa na kuteswa,
hata hivyo hakufungua kinywa chake;
aliongozwa kama mwana-kondoo
apelekwaye machinjoni,
kama vile kondoo anyamazavyo mbele ya wao wamkataye manyoya,
hivyo hakufungua kinywa chake.
8 cKwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa.
Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?
Kwa maana alikatiliwa mbali na nchi ya walio hai,
alipigwa kwa ajili ya makosa ya watu wangu.
9 dWakamfanyia kaburi pamoja na waovu,
pamoja na matajiri katika kifo chake,
ingawa hakutenda jeuri,
wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
10 eLakini yalikuwa ni mapenzi ya Bwana
kumchubua na kumsababisha ateseke.
Ingawa Bwana amefanya maisha yake
kuwa sadaka ya hatia,
ataona uzao wake na kuishi siku nyingi,
nayo mapenzi ya Bwana yatafanikiwa mkononi mwake.
11 fBaada ya maumivu ya nafsi yake,
ataona nuru ya uzima na kuridhika;
kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki
atawafanya wengi kuwa wenye haki,
naye atayachukua maovu yao.
Copyright information for
SwhNEN