‏ Isaiah 50:5-9

5 a Bwana Mwenyezi amezibua masikio yangu,
nami sikuwa mwasi,
wala sikurudi nyuma.
6 bNiliwapa mgongo wangu wale wanipigao,
mashavu yangu wale wangʼoao ndevu zangu;
sikuuficha uso wangu kutokana na fedheha
na kutemewa mate.
7 cKwa sababu Bwana Mwenyezi ananisaidia,
sitatahayarika.
Kwa hiyo nimekaza uso wangu kama jiwe la gumegume,
nami ninajua sitaaibika.
8 dYeye anipatiaye haki yangu yu karibu.
Ni nani basi atakayeleta mashtaka dhidi yangu?
Tukabiliane uso kwa uso!
Mshtaki wangu ni nani?
Ni nani aliye mshtaki wangu?
9 eNi Bwana Mwenyezi anisaidiaye mimi.
Ni nani huyo atakayenihukumu?
Wote watachakaa kama vazi,
nondo watawala wawamalize.
Copyright information for SwhNEN