‏ Isaiah 5:5-6

5 aSasa nitawaambia lile nitakalolitendea
shamba langu la mizabibu:
Nitaondoa uzio wake,
nalo litaharibiwa,
nitabomoa ukuta wake,
nalo litakanyagwa.
6 bNitalifanya nchi ya ukiwa isiyokaliwa na watu,
halitakatiwa matawi wala kulimwa,
nayo michongoma na miiba itamea huko,
nitaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.”
Copyright information for SwhNEN