‏ Isaiah 5:24-25


24 aKwa hiyo, kama ndimi za moto zirambavyo nyasi,
na kama vile majani makavu yazamavyo katika miali ya moto,
ndivyo mizizi yao itakavyooza
na maua yao yatakavyopeperushwa kama mavumbi;
kwa kuwa wameikataa sheria ya Bwana Mwenye Nguvu Zote
na kulisukumia mbali neno la Aliye Mtakatifu wa Israeli.
25 bKwa hiyo hasira ya Bwana inawaka dhidi ya watu wake,
mkono wake umeinuliwa na anawapiga.
Milima inatetemeka,
maiti ni kama takataka kwenye barabara.

Hata kwa haya yote, hasira yake haijageukia mbali,
mkono wake bado umeinuliwa juu.
Copyright information for SwhNEN