‏ Isaiah 49:24-26


24 aJe, nyara zaweza kuchukuliwa kutoka kwa mashujaa wa vita,
au mateka kuokolewa kutoka kwa watu wakali?
25 bLakini hili ndilo asemalo Bwana:

“Naam, mateka watachukuliwa kutoka kwa mashujaa,
na nyara zitapokonywa kutoka kwa watu wakali.
Nitashindana na wale wanaoshindana nawe,
nami nitawaokoa watoto wako.
26 cNitawafanya wale wanaokuonea kula nyama yao wenyewe,
watalewa kwa damu yao wenyewe,
kama vile kwa mvinyo.
Ndipo wanadamu wote watajua
ya kuwa Mimi, Bwana, ni Mwokozi wako,
Mkombozi wako, niliye Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.

Everyone uses cookies. We do too! Cookies are little bits of information stored on your computer which help us give you a better experience. You can find out more by reading the STEPBible cookie policy.