‏ Isaiah 43:22-24


22“Hata hivyo hukuniita mimi, ee Yakobo,
hujajitaabisha kwa ajili yangu, ee Israeli.
23 aHujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,
wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.
Sikukulemea kwa sadaka za nafaka
wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba.
24 bHukuninunulia uvumba wowote wenye manukato,
wala hukunipa kwa ukarimu
mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.
Lakini umenilemea kwa dhambi zako,
na kunitaabisha kwa makosa yako.

Copyright information for SwhNEN
The selected Bible will not be clickable as it does not support the Vocabulary feature. The vocabulary is available by hovering over the verse number.