‏ Isaiah 41:10-14

10 aHivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

11 b“Wote walioona hasira dhidi yako
hakika wataaibika na kutahayarika,
wale wakupingao
watakuwa kama vile si kitu, na kuangamia.
12 cIngawa utawatafuta adui zako,
hutawaona.
Wale wanaopigana vita dhidi yako
watakuwa kama vile si kitu kabisa.
13 dKwa maana Mimi ndimi Bwana, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
14 eUsiogope, ee Yakobo uliye mdudu,
ee Israeli uliye mdogo,
kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema Bwana,
Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Copyright information for SwhNEN