‏ Isaiah 37:24-25

24 aKupitia kwa wajumbe wako
umelundika matukano juu ya Bwana.
Nawe umesema,
‘Kwa magari yangu mengi ya vita,
nimepanda juu ya vilele vya milima,
vilele vya juu sana katika Lebanoni.
Nami nimeiangusha mierezi yake mirefu,
misunobari yake iliyo bora sana.
Nimefikia sehemu zake zilizoinuka juu sana,
misitu yake iliyo mizuri sana.
25 bNimechimba visima katika nchi za kigeni
na kunywa maji yake.
Kwa nyayo za miguu yangu
nimekausha vijito vyote vya Misri.’
Copyright information for SwhNEN