‏ Isaiah 34:2-8

2 a Bwana ameyakasirikia mataifa yote;
ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote.
Atawaangamiza kabisa,
atawatia mikononi mwa wachinjaji.
3 bWaliouawa watatupwa nje,
maiti zao zitatoa uvundo,
milima itatota kwa damu zao.
4 cNyota zote za mbinguni zitayeyuka
na anga litasokotwa kama kitabu,
jeshi lote la angani litaanguka
kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu,
kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini.

5 dUpanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni,
tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu,
wale watu ambao nimeshawahukumu,
kuwaangamiza kabisa.
6 eUpanga wa Bwana umeoga katika damu,
umefunikwa na mafuta ya nyama:
damu ya kondoo na mbuzi,
mafuta kutoka figo za kondoo dume.
Kwa maana Bwana ana dhabihu huko Bosra,
na machinjo makuu huko Edomu.
7 fNyati wataanguka pamoja nao,
ndama waume na mafahali wakubwa.
Nchi yao italowana kwa damu,
nayo mavumbi yataloa mafuta ya nyama.

8 gKwa sababu Bwana anayo siku ya kulipiza kisasi,
mwaka wa malipo,
siku ya kushindania shauri la Sayuni.
Copyright information for SwhNEN