Isaiah 28:1-3
Ole Wa Efraimu
1 aOle kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,
uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:
kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo!
2 bTazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.
Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,
kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,
atakiangusha chini kwa nguvu.
3 cLile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,
kitakanyagwa chini ya nyayo.
Copyright information for
SwhNEN