‏ Isaiah 24:21-23


21 aKatika siku ile Bwana ataadhibu
nguvu zilizoko mbinguni juu,
na wafalme walioko duniani chini.
22 bWatakusanywa pamoja
kama wafungwa waliofungwa gerezani,
watafungiwa gerezani
na kuadhibiwa baada ya siku nyingi.
23 cMwezi utatiwa haya, nalo jua litaaibishwa;
kwa maana Bwana Mwenye Nguvu Zote atawala
juu ya Mlima Sayuni na katika Yerusalemu,
tena mbele ya wazee wake kwa utukufu.
Copyright information for SwhNEN