‏ Isaiah 24:18-22

18 aKila akimbiaye asikiapo sauti ya hofu
atatumbukia shimoni,
naye yeyote apandaye kutoka shimoni,
atanaswa kwenye mtego.

Malango ya gharika ya mbinguni yamefunguliwa,
misingi ya dunia inatikisika.
19 bDunia imepasuka,
dunia imechanika,
dunia imetikiswa kabisa.
20 cDunia inapepesuka kama mlevi,
inayumbayumba kama kibanda kwenye upepo;
imelemewa sana na mzigo wa hatia ya uasi wake
na ikianguka kamwe haitainuka tena.

21 dKatika siku ile Bwana ataadhibu
nguvu zilizoko mbinguni juu,
na wafalme walioko duniani chini.
22 eWatakusanywa pamoja
kama wafungwa waliofungwa gerezani,
watafungiwa gerezani
na kuadhibiwa baada ya siku nyingi.
Copyright information for SwhNEN