Isaiah 2:17-21
17 a bMajivuno ya mwanadamu yatashushwa,na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,
Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
18 cnazo sanamu zitatoweka kabisa.
19 dWatu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,
na kwenye mahandaki ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia.
20 eSiku ile, watu watawatupia
panya na popo
sanamu zao za fedha na za dhahabu,
walizozitengeneza ili waziabudu.
21 fWatakimbilia kwenye mapango miambani
na kwenye nyufa za miamba
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia.
Copyright information for
SwhNEN