Isaiah 2:12-17
12 a Bwana Mwenye Nguvu Zote anayo siku aliyoiweka akiba
kwa wote wenye kujivuna na wenye kiburi,
kwa wote wanaojikweza
(nao watanyenyekezwa),
13 bkwa mierezi yote ya Lebanoni iliyo mirefu sana,
na mialoni yote ya Bashani,
14 ckwa milima yote mirefu
na vilima vyote vilivyoinuka,
15 dkwa kila mnara ulio mrefu sana
na kila ukuta wenye ngome,
16 ekwa kila meli ya biashara, ▼
na kila chombo cha baharini cha fahari.
17 g hMajivuno ya mwanadamu yatashushwa,
na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,
Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo,
Copyright information for
SwhNEN