‏ Isaiah 19:6-9

6 aMifereji itanuka;
vijito vya Misri vitapungua
na kukauka.
Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7 bpia mimea iliyoko kando ya Mto Naili,
pale mto unapomwaga maji baharini.
Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka,
litapeperushwa na kutoweka kabisa.
8 cWavuvi watalia na kuomboleza,
wale wote watupao ndoano katika Mto Naili,
watadhoofika kwa majonzi.
9 dWale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa,
wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.
Copyright information for SwhNEN