‏ Isaiah 19:11-16


11 aMaafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa,
washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga.
Unawezaje kumwambia Farao,
“Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima,
mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?

12 bWako wapi sasa watu wako wenye hekima?
Wao wakuonyeshe na kukufahamisha
ni nini Bwana Mwenye Nguvu Zote
amepanga dhidi ya Misri.
13 cMaafisa wa Soani wamekuwa wapumbavu,
viongozi wa Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
wamedanganyika,
walio mawe ya pembe ya taifa lake
wameipotosha Misri.
14 e Bwana amewamwagia
roho ya kizunguzungu;
wanaifanya Misri iyumbayumbe
katika yale yote inayoyafanya,
kama vile mlevi ayumbayumbavyo
katika kutapika kwake.
15 fMisri haiwezi kufanya kitu chochote,
cha kichwa wala cha mkia,
cha tawi la mtende wala cha tete.
16 gKatika siku ile Wamisri watakuwa kama wanawake. Watatetemeka kwa hofu mbele ya mkono wa Bwana Mwenye Nguvu Zote anaoinua dhidi yao.
Copyright information for SwhNEN