Isaiah 14:13-15
13 aUlisema moyoni mwako,“Nitapanda juu hadi mbinguni,
nitakiinua kiti changu cha enzi
juu ya nyota za Mungu,
nitaketi nimetawazwa
juu ya mlima wa kusanyiko,
kwenye vimo vya juu sana vya Mlima Mtakatifu.
14 bNitapaa juu kupita mawingu,
nitajifanya kama Yeye Aliye Juu Sana.”
15 cLakini umeshushwa chini hadi kuzimu,
hadi kwenye vina vya shimo.
Copyright information for
SwhNEN