Isaiah 13:3-5
3 aNimewaamuru watakatifu wangu;nimewaita mashujaa wangu waitimize hasira yangu:
wale wanaoshangilia ushindi wangu.
4 bSikilizeni kelele juu ya milima,
kama ile ya umati mkubwa wa watu!
Sikilizeni, makelele katikati ya falme,
kama mataifa yanayokusanyika pamoja!
Bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya
jeshi kwa ajili ya vita.
5 cWanakuja kutoka nchi za mbali sana,
kutoka miisho ya mbingu,
Bwana na silaha za ghadhabu yake,
kuangamiza nchi yote.
Copyright information for
SwhNEN