Isaiah 11:1-5
Tawi Kutoka Kwa Yese
1 aChipukizi litatokea kutoka shina la Yese,kutoka mizizi yake Tawi litazaa tunda.
2 bRoho wa Bwana atakaa juu yake,
Roho wa hekima na wa ufahamu,
Roho wa shauri na wa uweza,
Roho wa maarifa na wa kumcha Bwana
3 cnaye atafurahia kumcha Bwana.
Hatahukumu kwa yale ayaonayo kwa macho yake,
wala kuamua kwa yale ayasikiayo kwa masikio yake,
4 dbali kwa uadilifu atahukumu wahitaji,
kwa haki ataamua wanyenyekevu wa dunia.
Ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake,
kwa pumzi ya midomo yake atawaua waovu.
5 eHaki itakuwa mkanda wake
na uaminifu utakuwa mshipi kiunoni mwake.
Copyright information for
SwhNEN