‏ Hosea 9:3-9

3 aHawataishi katika nchi ya Bwana,
Efraimu atarudi Misri
na atakula chakula
kilicho najisi huko Ashuru.
4 bHawatammiminia Bwana sadaka ya divai
wala dhabihu zao hazitampendeza.
Dhabihu kama hizo zitakuwa kwao
kama mkate wa waombolezaji;
nao wote wazilao watakuwa najisi.
Chakula hiki kitakuwa kwa ajili yao wenyewe;
kisije katika Hekalu la Bwana.

5 cMtafanya nini katika siku ya sikukuu zenu zilizoamriwa,
katika siku za sikukuu za Bwana?
6 dHata ikiwa wataokoka maangamizi,
Misri atawakusanya,
nayo Memfisi
Memfisi kwa Kiebrania ni Nofu.
itawazika.
Hazina zao za fedha zitasongwa na michongoma,
nayo miiba itafunika mahema yao.
7 fSiku za adhabu zinakuja,
siku za malipo zimewadia.
Israeli na afahamu hili.
Kwa sababu dhambi zenu ni nyingi sana
na uadui wenu ni mkubwa sana,
nabii anadhaniwa ni mpumbavu,
mtu aliyeongozwa na Mungu
anaonekana mwendawazimu.
8 gNabii, pamoja na Mungu wangu,
ndiye mlinzi juu ya Efraimu,
hata hivyo mitego inamngojea
katika mapito yake yote,
na uadui katika nyumba ya Mungu wake.
9 hWamezama sana katika rushwa,
kama katika siku za Gibea.
Mungu atakumbuka uovu wao
na kuwaadhibu kwa ajili ya dhambi zao.
Copyright information for SwhNEN