Hosea 9:11-17
11 aUtukufu wa Efraimu utaruka kama ndege:hakuna kuzaa, hakuna kuchukua mimba,
hakuna kutunga mimba.
12 bHata wakilea watoto,
nitamuua kila mmoja.
Ole wao
nitakapowapiga kisogo!
13 cNimemwona Efraimu, kama Tiro,
aliyeoteshwa mahali pazuri.
Lakini Efraimu wataleta
watoto wao kwa mchinjaji.”
14 dWape, Ee Bwana,
je, utawapa nini?
Wape matumbo ya kuharibu mimba
na matiti yaliyokauka.
15 e“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali,
niliwachukia huko.
Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi,
nitawafukuza katika nyumba yangu.
Sitawapenda tena,
viongozi wao wote ni waasi.
16 fEfraimu ameharibiwa,
mzizi wao umenyauka,
hawazai tunda.
Hata kama watazaa watoto,
nitawachinja watoto wao
waliotunzwa vizuri.”
17 gMungu wangu atawakataa
kwa sababu hawakumtii;
watakuwa watu wa kutangatanga
miongoni mwa mataifa.
Copyright information for
SwhNEN