‏ Hosea 8:1-12

Israeli Kuvuna Kisulisuli

1 a“Wekeni tarumbeta midomoni mwenu!
Tai yuko juu ya nyumba ya Bwana
kwa sababu watu wamevunja Agano langu,
wameasi dhidi ya sheria yangu.
2 bIsraeli ananililia,
‘Ee Mungu wetu, tunakukubali!’
3 cLakini Israeli amekataa lile lililo jema,
adui atamfuatia.
4 dWanaweka wafalme bila idhini yangu,
wamechagua wakuu bila kibali changu.
Kwa fedha zao na dhahabu
wamejitengenezea sanamu kwa ajili
ya maangamizi yao wenyewe.
5 eEe Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama!
Hasira yangu inawaka dhidi yao.
Watakuwa najisi mpaka lini?
6 fZimetoka katika Israeli!
Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu.
Atavunjwa vipande vipande,
yule ndama wa Samaria.

7 g“Wanapanda upepo
na kuvuna upepo wa kisulisuli.
Bua halina suke,
halitatoa unga.
Kama lingetoa nafaka,
wageni wangeila yote.
8 hIsraeli amemezwa;
sasa yupo miongoni mwa mataifa
kama kitu kisicho na thamani.
9 iKwa kuwa wamepanda kwenda Ashuru
kama punda-mwitu anayetangatanga peke yake.
Efraimu amejiuza mwenyewe
kwa wapenzi.
10 jIngawa wamejiuza wenyewe miongoni mwa mataifa,
sasa nitawakusanya pamoja.
Wataanza kudhoofika chini ya uonevu
wa mfalme mwenye nguvu.

11 k“Ingawa Efraimu alijenga madhabahu nyingi
kwa ajili ya sadaka za dhambi,
hizi zimekuwa madhabahu
za kufanyia dhambi.
12 lNimeandika kwa ajili yao mambo mengi
kuhusu sheria yangu,
lakini wameziangalia
kama kitu cha kigeni.
Copyright information for SwhNEN