Hosea 14:5-7
5 aNitakuwa kama umande kwa Israeli;atachanua kama yungiyungi.
Kama mwerezi wa Lebanoni
atashusha mizizi yake chini;
6 bmatawi yake yatatanda.
Fahari yake itakuwa kama mti wa mzeituni,
harufu yake nzuri kama mwerezi wa Lebanoni.
7 cWatu wataishi tena kwenye kivuli chake.
Atastawi kama nafaka.
Atachanua kama mzabibu,
nao umaarufu wake utakuwa
kama divai itokayo Lebanoni.
Copyright information for
SwhNEN