Hosea 10:5
5 aWatu wanaoishi Samaria huogopakwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni. ▼
▼Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.
Watu wake wataiombolezea,
vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,
wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,
kwa sababu itaondolewa kutoka kwao
kwenda uhamishoni.
Copyright information for
SwhNEN